MWAKA WA 2010 TUPAMBANIE MAISHA BORA KWA KILA MKENYA
Makala ya Nguvu ya Hoja kwa KSB: Januari 1, 2010
na Ndugu Mwandawiro Mghanga

Baada ya pilkapilka za sherehe za Krismasi, sasa tumefikisha mwaka mpya wa 2010. Je, mwaka wa 2010 utakuwa mwaka wa heri na fanaka? Kwani mwaka wa 2009 nitauweka katika fungu la miaka mibaya zaidi niliyoishuhudia katika uhai wangu.
Kwanza ni kwa sababu za kibinafsi. Kwani mnamo Oktoba 26 mwaka huu nilimpoteza mama yangu mzazi na mpendwa, Alice Mafundisho Mghanga. Pamoja na yote aliyonifanyia kama mwanaye, pia namkumbuka na kumuenzi mama yangu kwani alitoa mchango wake katika harakati za kupambania demokrasi nchini. Mama yangu alishuhudia watoto wake wote wa kiume wakisakwa, wakikamatwa, wakiteswa na kufungwa na serikali ya imla ya Moi na KANU. Mama yangu alilazimika kutumia muda mrefu wa machungu kusafiri kutoka Werugha kwenda kupambana kutuoana jela Kamiti, Eldoret na Kisumu. Pamoja na hayo, wakati wote alinitia moyo kuendelea na mapambano aliyoyaona kuwa ya haki na kimaendeleo. Ndiyo kwa maana nachukua fursa hii kuwatambua kina mama pahali popote walipo nchini katika juhudi zao za kila siku za kupigania maisha bora na ya kiutu kwa jamaa zao na jamii pia.
Mwaka wa 2009, mabadiliko ya hali ya hewa yaliathiri vibaya kila sehemu na jamii Kenya: mvua haikunyesha jinsi ilivyokuwa imetabiriwa na wataalamu wa hali ya hewa; kilimo kilifeli kwa kuzidi kwa ukame; maelfu ya mifugo ilikufa kwa kukosa malisho na maji na jamii za wafugaji sasa zinadorora kwa kukosa lishe, dhiki na ufukara; chemichemi za maji zilipotea huku mito ikikauka; wanyamapori pia walikufa kwa njaa na kiu; vita kati ya binadamu na wanyamapori viliongezeka; usalama ulizoroteka huku vita vya kikabila vya kuibiana mifugo na kushindania maliasili vikiongezeka; umeme ulipungua na kughalika; ufukara ulikua kila siku miongoni mwa umma; uhalifu ukazidi huku uchumi ukidorora. Huku tukielekea mwaka wa 2010, lazima tukumbushane kuwa swala la uhifadhi wa mazingira ni la kufa na kupona linalohitaji mchango wa kila mtu. Inasikitisha kuwa kongamano la kimataifa kuhusu mazingira lililofanyika nchini Denmark mwaka huu huu, lilihujumiwa na serikali za kibeberu na kushindwa kukubaliana kuhusu mikakati halisi ya kisheria ya kupunguza athari hatari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Pamoja na kwamba mvua sasa inanyesha katika sehemu nyingi nchini, njaa bado ni mtikisiko wa kitaifa. Hili linasikitisha. Tena linaaibisha. Na kisha linakasirisha. Mamilioni ya Wakenya kote nchini wanakabiliwa na baa ya njaa. Hata wengine tayari wamekufa kwa njaa. Hivi sasa serikali ambayo imekuwa ikichapa siasa duni na kulala usingizi wa pono huku tatizo hili likikua inababaika na suluhisho za wazima moto. Ni kana kwamba njaa hii imetokea ghafla bin vu. Na ukweli ni kwamba njaa imekuwa nasi wakati wote.
Ni watu wachache tu nchini ambao wana lishe bora na ya kutosha kila mara. Idadi kubwa ya Wakenya siku zote wanadorora katika dhiki, ufukara na ukosefu. Ingawa tatizo la njaa limezidi na kujidhihirisha zaidi nchini kuliko wakati mwingine wowote, si lipya katika mitaa ya mabanda mijini, watu wa jamii za wachungaji na sehemu kame za nchi. Maskwata, wakimbizi ndani ya nchi, wachuuzi, wafanyikazi wa ngazi za chini na wakulima makabwela, hawali wakashiba, sembuse lishe bora. Je, serikali ina mikakati gani halisi na endelezi la kufukuza njaa kabisa nchini mnamo 2010?
Jambo la kutia moyo ni kwamba Katiba Mpya ya Kitaifa itapatikana mwaka 2010. Nina matumaini hayo. Wala sioni kwa nini Kenya ishindwe kuipata wakati huu. Maana kwa kweli Rasimu ya Katiba inayoendelea kupigwa msasa hivi sasa na washikadau wa kila aina wenye nia njema, inakaribia kabisa kile ambacho kimetarajiwa na Wakenya kwa muda mrefu. Wala hatuwezi kupata katiba kamilifu kwani mja si mkamilifu. Pamoja na hayo sina budi kukariri ukweli wa mambo: Katiba Mpya si maisha mapya bali ikiwa nzuri inaweza kuwa ngazi ya kuwania maisha mapya. Hii inategemea siasa na harakati za kitabaka. Maana siasa na harakati za kitabaka ni mama wa mambo yote, yawe ya kisiasa, kiuchumi, kibiashara, kijamii, kitamaduni na ya kila hali.
Ili kuwe na maisha mapya mnamo 2010 lazima Kenya ibadilike kisiasa, kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kwa kila hali. Maana siasa mbaya za kibepari hazitatafsiri Katiba Mpya kuboresha maisha ya wengi. Tukumbuke kuwa wanasiasa watakaodhibiti nguvu za Dola na Serikali ndiyo vilevile watakaotafsiri na kutekeleza Katiba Mpya. Nao watatafsiri na kutekeleza Katiba ili kutosheleza masilahi yao ya kiuchumi, kibiashara, kiitikadi na kitabaka. Wakati tukielekea 2010 na hatimaye 2012 tuwe tunakumbushana kuwa watuhumiwa wa wizi, utapeli, ufisadi, mauaji na uhalifu wa kila aina wakiendelea kuongoza nchi hii wataendelea kutafsiri na kutekeleza Katiba Mpya kulinda uhalifu wao tu. Watatunga sheria za kuhakikisha mfumo unyonyaji, udhalimu na ufisadi unaendelea chini ya Katiba Mpya.
Aidha, tusisahau kuwa maongozi mabaya yametufikisha katika hali ambapo tumepoteza uhuru wa kitaifa na kuingiliwa na ubeberu hadi uvungoni. Inasikitisha kuwa Wakenya wengi leo wanaamini watapata haki zaidi kutoka kwa mahakama na sheria za kibeberu, kama za The Hague, kuliko kutoka kwa tasisi zao wenyewe za haki. Hali hii ni mbaya na ya kuogofya. Lakini watu watakuwaje na imani na uongozi wa ulafi wa kuwanyonya, kuwanyanyasa, kuwafukarisha na wa kulinda wahalifu ili kuendelea kuwa uongozini baada 2012? Tunapouwacha mwaka 2009 huku tukielekea 2010 tukumbushane kuwa uongozi utakaorudisha hadhi na uhuru wa nchi yetu ni ule utakaowasikiliza Wakenya, kulinda haki zao za kidemokrasi na kibinadamu na kujenga mfumo wa kiuchumi unaozingatia masilahi ya kila mtu nchini. Na ili kuleta uongozi bora nchini, sharti kila Mkenya awajibike, tupambane kuondoa maovu yote yaliyokuwako mnamo 2009. Kisha 2010 tuungane pasina kujali kabila, umri au jinsia kupambania Kenya itakayohakikisha kuwa rasilimali za kitaifa zinatumika kuboresha maisha ya kila Mkenya.
Mwandawiro Mghanga, Barua pepe: mwandawiro2002(at)yahoo.com
By NICHOLAS NGOLYOPosted Wednesday, January 6 2010 at 15:35
A British Army officer on Wednesday denied assaulting a senior police officer and using derogatory words against him.
He is alleged to have called the officer a “black monkey.”
David Robins was arraigned before Kibera senior principal magistrate Grace Nzioka under tight security.
But the army man denied two charges of assault and creating a disturbance. He was released on a Sh50,000 bond with a surety of similar amount.
Mrs Nzioka also ordered Mr Robins, attached to Kifaru Barracks, to deposit his passport with the court. The case will be heard on March 16.
The prosecutor, chief inspector Francis Ndiema told the court on January 5 at Parklands Ojijo Roundabout, Nairobi, that the Briton unlawfully assaulted the Officer in-charge of Parklands (OCS), Chief Inspector Stephen Okal.
The court heard that at the time of the said assault the OCS was acting in due of execution of his duty.
Another charge stated that the accused created disturbance in a manner likely to cause a breach of the peace by using racist remarks “…….black monkey” to Mr Okal at the time of execution of his duty.
The police claims that the accused was driving on the wrong side on Limuru road towards the roundabout when he was stopped only to hurl abuse at the police.
In another incident in neighbouring Tanzania last December, a Canadian diplomat was recalled after he spat at a policeman directing traffic on a busy intersection.
Tanzanian media reported that ‘angered’ by a traffic jam, the envoy opened his car window and spat at the policeman.
The Foreign ministry said the incident was a humiliation, not just to the police officer but the entire country as well.
Add a comment (12 comments so far)
You need to login first to submit a comment.
Submitted by bsaoke
Posted januari 06, 2010 10:24 PM
If the mzungu did exactly the same thing in the UK to a any black policeman, he would be jailed, no kidding. But don’t forget that is Kenya… some junior diplomat from the High Commission will go to Wetangula and the criminal will go scot free
Submitted by The_Reformer
Posted januari 06, 2010 10:23 PM
You know why this guys do it? Because we are Stupid.Yes, we allow them to order us around even after ‘independence, we go with begging bowls for funding, and they know we can’t a damn thing about it.WHo says we are free? why are we still in the commonwealth?How can you keep friends with someone who attacked you, raped your wife and humiliated you?The Brits are good at what they call’winning hearts and minds’We need to wake up as Africans.
Submitted by pinakin
Posted januari 06, 2010 08:30 PM
In reply to mhd. It is prudent to check all facts before critisizing the kenyan security forces. The british are not a backbone of kenyan security. They only train in kenya. If they cannot respect the country then they should be told to leave.