Makala ya Nguvu ya Hoja, KSB Jumapili Machi 14, 2010
na Ndugu Mwandawiro Mghanga

Kiongozi ambaye aneweza kuwa katika msitari wa mbele wa kupambana dhidi ya ufisadi ni yule aliye msafi kabisa mbele ya ufisadi. Ni mtu yule ambaye haogopi vita hivi maana hajawahi kushiriki katika ufisadi kwa njia yoyote ile. Tena awe ni mzalendo, mkweli na mtu mwenye utu ambaye amejikomboa kutoka kwa vishawishi vya tamaa za ulimbikizaji wa pesa na mali za binafsi ambazo anazitumia kuwatawala, kuwadanganya, kuwanyonyanya na kuwanyanyasa wengine.
Mtu ambaye anaweka masilahi ya kitaifa mbele na anaeishi ili kuishi ili kuboresha maisha ya kila Mkenya kwa kutumia mamlaka aliyo nayo kupigania uhuru, usawa, haki na ukombozi wa taifa lake, huyo anaweza kutegemewa kuongoza mapambano dhidi ya adui ufisadi. Aidha, shujaa wa vita dhidi ya ufisadi anahitajika kuwa jasiri, mtu ngangari, ambaye wakati wowote ako tayari na mbioni kuutafuta na kuupiga vita popote ufisadi popote pale unapojitokeza, hata kama u miongoni mwa watu anaohusiana nao kiukoo, kikabila, kidini, kisiasa au kirafiki. Je, nani katika serikali inayotawala anaweza kuwa shujaa wa kupambana dhidi ya ufisadi kwa kutumia vigezo hivi?
Nchi hii inaendelea kukumbwa na kashafa juu ya kashfa ya ufisadi. Viongozi ambao ndiyo wanaostahili kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi wenyewe wanatajwa kuhusika na ufusadi siku nenda siku rudi. Kila kunapokucha kunatokea kashfa mpya ya ufisadi ambayo inawahusu viongozi wa ngazi za juu za serikali. Na kila mara wanaotajwa kwa ufisadi na vyombo vya serikali vyenyewe vya kupambana dhidi ya ufisadi wanaita vyombo vya habari kulalamika kwa kusingiziwa ufisadi kwa sababu za kisiasa.
Yaani watu wanajificha ndani ya vyombo vya habari, siasa na kabila zao kujitetea kutoka kwa lawama za kushiriki ufisadi. Kisha wanaendelea tu kuwa viongozi. Taarifa za Tume ya Kenya ya Kupambana dhidi ya Ufisadi zinaendelea kuwa tamthilia na kelele za chura ambazo hazimzuii ng’ombe kunywa maji. Vilevile ni vilemba vya ukoka vinavyovishwa wananchi wanaotarajia ukweli na haki itendwe na serikali hii kuhusu ufisadi.
Ni nchi gani ulimwenguni ambapo Waziri Mkuu mwenyewe anataja baadhi ya mawaziri kuwa watuhumiwa wa ufisadi kisha akaamru wawachishwe kazi kwa muda lakini mawaziri hao wakakataa katakata kujiuzulu tena kwa kiburi na bezo? Aidha, mawaziri wenyewe wanaendelea na kazi zao za uwaziri huku wakijigamba na kujitapa mbele ya umma, hasa wa kabila zao, kuwa mashujaa? Mashujaa wa nani na nini? Mashujaa wa kabila zao, na vyama vyao na wa kuasi waziri mkuu kwa kuendelea kuwa mawaziri hata baada ya kutuhumiwa katika kashfa za ufisadi katika wizara zao.
Naye waziri mkuu anaanza vita dhidi ya ufisadi na kuviwachia njiani? Ikiwa kweli anaamini hao mawaziri wake ni watuhumiwa wa ufisadi, mbona amekubali waendelee kuwa mawaziri katika serikali ambayo tunaambiwa anaisimamia? Kwani akubali wakaidi amri yake? Haitoshi kutuambia ati ni kupuuzwa kwa agizo lake na Rais ambako kumehujumu juhudi zake za kuwaondoa mawaziri watuhumiwa hao. Je, sisi wananchi tuendelee kuvumilia kuoongozwa na watuhumiwa wa wizi kwa vile Rais amehujumu juhudi za waziri mkuu za kuwachukulia hatua?
Maji ukiyavulia nguo, bwana waziri mkuu, sharti uwe tayari kuyaoga. Maana kutuambia fulani ni watuhumiwa wa ufisadi ambao wanapaswa kufutwa kazi, hata angalawa kwa muda, ili uchuguzi ufanyike, halafu unawainulia mikono na kukubali kuendelea kuwa nao katika serikali yako na chama chako, hakika kunawapa wananchi mashaka makubwa. Ni kama kutuambia viongozi mmeshindwa kabisa na vita dhidi ya ufisadi na kwa hivyo hatuna budi ila kuendelea kukubali au kuvumilia kuongozwa na wezi. Na hili ni hatari kwa usalama na maendeleo ya kitaifa. Ndiyo kwa maana hatutakubali kuwacha vita dhidi ya mbea ufisadi kwa kuwa tukifanya hivyo tutamalizika kabisa.
Kisha tukishangazwa na ya Musa yanazuka ya Firauni. Kashfa nyingine ya ufisadi unaohusu viongozi na ardhi ya makaburi inazungumziwa jijini sasa. Na wimbo ni ule ule tu wa siku zote. Wanaoshukiwa wanajitetea kupitia kwa vyombo vya habari wakidai kuna njama za kisiasa za kutaka kuwamaliza. Nami nashindwa tena, je mambo ya ukweli, haki na sheria yanapatikana kwa magazeti, redio na runinga au mahakamani? Ada ya mja hunena mungwana ni vitendo, ikiwa jina lako limeharibiwa kwa kusingiziwa uongo mbona usiende kulisafisha mahakamani? Washtaki hao watu wanaokuharibia jina bure na udai fidia kutoka kwao? Unaogopa nini?
Maana kukataa kwenda mahakamani na badala yake kuchagua kulia na kujipiga kifua kadamnasi ya vyombo vya habari kunatufanya tushuku kuwa kuna kitu unaogopa. Ndiyo mimi husema, mshahara unaopokea pamoja na marupurupu yake yanatosha. Isitoshe, wengi wa viongozi wanaotajwa kwa kashfa za ufisadi tayari ni mamilionea na hata mabilionea. Mbona hamtosheki jamamani na hamtaishi ulimwengini milele? Mbona hamhurumii watu wenu ambao wengi ni mafukara kupinfukia? Kwa nini mnajitumbukiza katika hali ambapo mnaishi katika nyuma za glasi huku mnarushia wengine mawe. Au mnaogopa kuwarushia mawe maana mnaishi katika nyumba za glasi!
Kwa Rais Kibaki na Waziri Mkuu Raila naendelea kukariri lazima muwajibike: mawaziri wanaotuhumiwa kushiriki wizi wanga’tuke ama wang’atuliwe. Kuendelea kukubali watuhumiwa wizi wa mali ya umma kuendelea kushikilia nyadhifa za uongozi wa kitaifa ni kupalilia na kutilia mbolea uhalifu. Wala haiwezi kuwa vingine. Aidha, serikali ambayo inalinda wahalifu siyo tu haiwezi kuaminika bali pia inaaibisha nchi yetu na kuhujumu juhudi za wananchi za kujikomboa kutoka kwa umaskini ambao unakua siku nenda siku rudi. Ukweli na uambwe!
Mwandawiro Mghanga, Barua pepe: mwandawiro2002(at)yahoo.com
Ndugu mwandawiro !
umetoboa siri kwa kiswahili fasaha na nadhifu !
asante baba
I appreciate and understand that Swahili is our national language, but this guys articles make very very tiresome reading. Kwani he cant switch to English? Swahili sanifu is a rare commodity for many, myself included (haha) and trying to read these kind of articles is just too tidious. Not that I’m being critical, rude or confrontational just real.
KSB: Swahili is a national language. If Kenyans are ready to learn Swedish and other languages, why not Swahili?
Kenya damu but abroad this time you got it wrong.Kiswahili is our national language and we must take pride in reading and understanding it.Too bad Ndugu Mghanga’s articles tire you,but some of us use them to polish our knowledge of the language and also appreciate the contents. Why would we learn so much Swedish that we are not exposed to while growing up at home, yet feel reading Kiswahili is tedious? Tuondoe kasumba ya ukoloni na tuendeleze Kiswahili.
Mr. kenya damu but abroad !
I guess you are a creapy, brain washed moron who cant speak english perfectly but with a luo accent,!
You cant speak swahili !!! my ass !
Suppose he is the presi,hakuna angemuelewa huyu mtu.
Dame !
nani angemuelewa nani ???
Presi una maana President (Raisi) au nani ?
Mtu anaongea kiswahili fasaha kila mtu atamuelewa !!