Makala ya Nguvu ya Hoja kwa KSB Jumapili Mei 9, 2010na Ndugu Mwandawiro Mghanga

Katika makala ya Jumapili hii nitagusia matekeo matatu muhimu yaliyofanyika ulimwenguni juma hili. Nitaanza na mbali, katika bara la Ulaya, Wingereza. Katika nchi hiyo kumefanyika uchaguzi wa kitaifa. Ni muhimu kutaja uchaguzi wa Wingereza kwani nchi hii ikiwa taifa kubwa la kibepari na kibeberu linaathiri sana maswala ya kimataifa. Na kutokana na uhusiano wa kikoloni ambao unaendelea hadi wa leo kati ya Afrika na Wingereza, Wakenya wengi wamekuwa wakifuatilia uchaguzi wa nchi hii kwa makini. Wingireza ni nchi yenye historia ndefu ya mfumo wa demokrasi ya kibepari.
Lakini ni demokrasi ambayo imepiga vita mfumo wa vyama vingi kwa kuubadilisha kuwa mfumo wa vyama vichache katika utekelezaji wake. Vyama vinavyoathiri maisha ya Wingereza ni vitatu tu, Labour Party (cha mlengo wa kushoto), Conservative Party (mlengo wa kulia) na Liberal Democrats (mlengo wa kulia vilevile). Ndiyo kwa mana nafurahi kuwa rasimu ya katiba ambayo natarajia itakuwa katiba mpya ya Kenya mwaka huu, inatilia manani mfumo wa vyama vingi vya kisiasa wala siyo vyama vichache tu.
Kuna watu nchini Kenya ambao hutamani mfumo wa vyama vichache kama huo unaotekelezwa Wingereza na Marekani. Lakini hao ni watu ambao hupuuza demokrasi na umuhimu wa sera na itikadi katika kujenga utamaduni wa kidemokrasi na haki za binadamu.
Tangu kishinde Conservative Party mara ya mwisho, chama Labour Party kimeshikilia hatamu za serikali kwa miaka 13 mfulizo. Kihistoria msingi wa labour Party ni tabaka la wafanyikazi na sera za kisoshalisti. Lakini tangu Waziri Mkuu Tony Blare achukue uongozi wa chama hicho na baadaye kurithiwa na rafiki yake Gordon Brown, chama hiki kimeshikilia kufuata mkondo wa kisiasa, kiuchumi na kisiasa wa vyama vya leba vya Ulaya, mkondo wakibepari.
Katika siasa za nchi za nje, chama cha Labour Party kimeshikilia sera za kibeberu na vita za kina George Bush, sera ambazo zimekuwa kikwazo cha amani ulimwenguni, hasa Mashariki ya Kati, Afghanistan na Pakistan. Ndiyo kwa maana vyama vya leba vya Ulaya vimekuwa vikipoteza wafuasi wao kwa vyama vya kibepari. Uchaguzi uliyofanyika Wingereza juma hili unadhihirisha ukweli huu: wananchi wa Wingereza hawaoni tofauti kati ya Conservative Party na Labour Party ya Tony Blare na Gordon Brown ambayo imetia fora katika kutekeleza sera za kubeparisha uchumi wa Wingereza. Ndiyo kwa maana wengi wao wakaamua “ukitaka kula nguruwe kula aliyenona” kwa kuchagua mabepari wenyewe hasa, Conservative Party. Kwa siasa za ndumulakuwili Labour Pary inazidi kupoteza imani kwa wananchi wa Wingereza.
Hapa Afrika, Nigeria ina tanzia kutokana na kifo cha Rais Umaru Yar’ Adua ambaye alifariki hivi majuzi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Hayati huyo alizikwa nyumbani kwao Alhamisi juma hili. Makala haya yanatuma rambirambi kwa jamaa ya marehemu na waNigeria. Wakati huo huo mwenye bahati kama jina lake, Goodluck Jonathan, aliyepanda kwa miujiza hadi akawa makamu wa Rais wa nchi hiyo, anazidi kubahatika kwa ndiye sasa Rais mpya wa Nigeria alieapishwa na kutawazwa jana.
Lazima tuwapongeze watu wa Nigeria kwa kufanya haya yote kwa amani na kwa misingi ya kisheria na kikatiba. Rais Goodluck Jonathan ana kibarua kikubwa alichowachiwa na hayati Yar’ Adua: kuongoza taifa lenye idadi kubwa ya watu zaidi Afrika na vilevile la watu weusi wengi zaidi ulimwenguni. Itampasa akabiliane na changamoto za kupambana na ufisadi, vita vya kidini na kikabila, umaskini miongoni mwa idadi kubwa zaidi ya raia na tisho la ugaidi. Kutokana na kutekeleza sera za kibepari na ukolonimamboleo, Nigeria ikiwa mojawapo wa nchi inayozalisha mafuta ya nishati mengi zaidi ulimwengini ndiyo vilevile inayokumbwa na ufukara na ukesefu wa nishati!
Wanaofaidi mafuta ya Nigeria si watu wa Nigeria bali ni makampuni ya kibepari ya kimataifa na mabwanyenye wa Nigeria, wengi wao wakiwa viongozi. Hali hii imesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Niger Delta, ambavyo havikomi. Yanayoendelea Nigeria ambayo sharti Rais Goodlauck Jonathan ayatafutie ufumbuzi mahususi yanatukumbusha Wakenya kuwa kabla ya kutekeleza sera za kuhakikisha kuwa jamii zinashirikishwa kikamilifu katika kuhifadhi na kupata faida za kiuchumi za rasilimali zao, hapawezi kuwa na amani wala maendele endelezi. Ninafurahi kuwa jambo hili limetiliwa manani na rasimu ya katiba mpya ya Kenya.
Tukirudi nyumbani, naona habari njema za kutupa moyo na matumaini. Safari ya kuelekea kwa katiba mpya ya kitaifa inaendelea sasa na karibu tutafika. Maana jana Mkuu wa Sheria alichapisha rasimu rasmi ya katiba na kuipatia tume huru ya muda ya kusimamia uchaguzi (IIEC). Kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu jana makundi mbalimbali yatazunguka kote nchini kuelimisha wananchi kuhusu kilichoko ndani ya rasimu ya katiba.
Kisha ndipo tutakapoingia katika kampeni kuhusu katiba. Inasikitisha kuwa kuna mamilioni ya Wakenya ambao bado hawajui kusoma na kuandika. Kutojua kusoma na kuandika ni kikwazo kikubwa kwa demokrasi na maendeleo na ni wajibu wetu tushughulikie tatizo hili kama taifa. Kwa sasa, watakaoendesha elimu na kampeni kuhusu rasimu ya katiba wana jukumu la kuwaeleza wenzetu ambao hawajui kusoma na kuandika ukweli jinsi ulivyo katika rasimu ya katiba yenyewe ili waweze kuamua kwa misingi ya ukweli.
Kwa wale ambao wanaipigia debe rasimu ya katiba ipite na kuwa katiba mpya mwaka huu, kama mimi, tufahamu kuwa tunakabiliwa na kibarua kikubwa cha kupambano na wanaoipinga rasimu hii. Lakini yote yafanyike kwa amani. Kuhonga watu kwa pesa katika uchaguzi ni dhambi, kosa na hujuma kwa kukua kwa demokrasi. Tayari pesa nyingi zimemwagwa na wapinzani wa katiba kuwaathiri watu wakatae rasimu ya katiba na hivyo watuzuie kupata katiba mpya.
Lazima vyombo vyote vinavyohusika vijitayarishe kuwachukulia hatua za kisheria watakaotumia hongo kama fimbo. Na wananchi wakumbuke wanaotumia pesa kuwashawishi watu kuwa upande wao hawana hoja za kupinga rasimu ya katiba. Nakariri: rasimu ya katiba si mbaya, tuipitishe iwe katiba kisha tuipige msasa baadaye.
Mwandawiro Mghanga, Barua pepe: mwandawiro2002(at)yahoo.com
Why do Kenyans generally think that others are idiots? “Ndugu” Mwandawiro never had any time for wanainchi or bothered to blog when he was MP. Nor did he preach this socialist and “ndugu” gospel then. Now that he is out of the system of “eating” he bombs KSB with propaganda. Kenyans arent fools and can see right through his “fake” politics. His has no credibiltity and is certainly not fooling anyone. Arudi mashabani akalime, hatutaki siasa za peni bili.
Ya Mumbi, I think Mwandawiro is doing what any politician ought to do – making new propaganda in readyness for next elections. He may vanish again after election but I think KSB is giving him publicity because the admin is an avowed Communist like him and birds of the same feathers flock together. KSB will give publicity to anybody supporting socialism in Kenya and I think Mwandawiro understands this. Osewe’s book is about “Stolen Presidency” but there is a lot of Communist ideas for Kenya. Let Mwandawiro spread his propaganda and the people of Kenya to decide!
while I do not agree with most of Mwandawiro propoganda, for those who followed his 5yrs term, he did alot,despite being under his Boss Nyachai. And believe me kenya need people like Mwandawiro and not Kiraitu and his likes.