Washoga wa Kenya Wafunga Ndoa
NDOA ya wanaume wawili wa Kenya iliyofungwa jijini London, Uingereza, ilizua gumzo la wiki nchini Uingereza, hususan miongoni mwa Wakenya wanaoishi Uingereza. Ndoa hiyo iliyofungwa Jumamosi ya Oktoba 17, mwaka huu, kati ya Bw Daniel Chege Gichia (39) na Charles Ngengi (40), jijini London. Hii ni ndoa ya kwanza ya mashoga wa Kenya kufungwa nchini Uingereza ambapo wote ni raia wa Kenya.
Timu ya takribani watu 20, wakiwamo wageni waalikwa, waliwasili katika Ukumbi wa Islington Town Hall. Sherehe hiyo iliwajumuisha wapambe wawili wanawake kutoka Kenya na wanaume wawili, mmoja wao akiwa aliwasili katika shughuli hiyo maalumu akitokea Uholanzi kwa ajili ya sherehe hiyo.
Shughuli hiyo iliyodumu kwa nusu saa iliendeshwa na msajili wa ndoa katika Baraza la Islington.
Sherehe za ndoa hiyo inayoelezwa kuwa haikuhudhuriwa na ndugu wa karibu wa familia zote mbili ilizua shutuma kali miongoni mwa raia wa Kenya wanaoishi Uingereza ambao walisema ni ushenzi ambao hawakubaliani nao.
NOTE: This story has been reported widely around the world and KS-beers can have their share in Kiswahili. SOURCE


